November 21, 2018

 
Ofisa habari wa timu ya Ruvu Shooting, Masau Bwire amesema kuwa wapo tayari kupindua meza kibabe mbele ya Azam FC katika mchezo wao wa kesho utakaochezwa uwanja wa Chamazi.
 

Azam FC ni vinara wa ligi baada ya kucheza michezo 12 bila kupoteza, watakutana na Ruvu Shooting ambao wao wamepoteza michezo 5.

Bwire amesema kuwa wana uzoefu na uwanja watakaoutumia hivyo kuwa kwao ugenini ni kukamilisha ratiba.


"Uwanja wa Azam FC ila tumeuzoea kutokana na kuchezea michezo mingi pale, hatuna wasiwasi tutaendeleza sera yetu ya kupapasa square, mashabiki watupe sapoti ya kutosha," alisema.


Ruvu Shootig wamecheza michezo 13 kwenye ligi wameshinda michezo 4 wakiwa na pointi 16 watapambana na Azam FC wenye pointi 30.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic