MZUNGU AMVAA KICHUYA SIMBA, AFUNGUKA NAMNA HII
Kocha Mkuu wa Simba, Mbelgiji Patrick Aussems, amefunguka kuwa kitendo cha Shiza Kichuya kutoanza kwenye michezo iliyopita si tatizo, bali ameamua kufanya hivyo ili kuona viwango vya waachezaji wake wengine.
Mchezo uliopita wa Simba na JKT Tanzania ambao ulipigwa kwenye Uwanja wa Mkwakwani jijini Tanga, Kichuya hakuweza kucheza mechi hiyo na alikuwa katika benchi.
Kichuya msimu huu umekuwa ni wa tofauti ukifananisha na msimu uliopita ambao alicheza takribani mechi 29 na zote alikuwa akianza huku akitoa zaidi ya asisti 25 za mabao chini ya Kocha Mfaransa, Pierre Lechantre.
Kwa mujibu wa Championi, Mbelgiji alisema haoni kama ni tatizo kwa Kichuya kuanzia benchi ila ameamua kuanza kujaribu kuangalia uwezo wa wachezaji wake.
“Kichuya si kwamba namuweka pembeni unajua katika kikosi changu hakuna mchezaji ambaye naweza kusema yeye kila siku atacheza kikosi cha kwanza, hapana ninachofanya kwa sasa nataka kuona kila mchezaji anapata nafasi pale ambapo anafanya vizuri katika mazoezi.
“Nafanya kama mzunguko kwa wachezaji kuona uwezo wa kila mmojawapo, hivyo suala la Kichuya kuanzia benchi kwangu siyo tatizo ni jambo la kawaida,” alisema Aussems.







Hivi hamnaga picha nyingine ya kichuya au
ReplyDeleteHuna akili..unajifanya mjanja kuandika vichwa vya habari vinavyomtega msomaji ile aifungua lakini akisoma habari anakuta maelezo tofauti..Sio sasa..huna maadili ya uandishi.Naenda shule kasome.Ukiandika hapa kuhusu Ajibu ni tofauti na unavyoabdika kuhusu Kichuya
ReplyDeleteWore tunajua maana ya kumvaa MTU..usituchezee akili
ReplyDeleteJe kitu gani kocha kamvaa Kichuya?
ReplyDeleteProtas-Iringa