NI MAAJABU, MPAKA SASA YANGA HAWAJUI WANAENDA KUFANYA UCHAGUZI UPI
Na George Mganga
Baadhi ya wanachama wa Yanga wamekuja na kali ya siku baada ya kusema hawajui ni uchaguzi upi wanaenda kufanya Januari 13 2018.
Hatua hiyo imekuja kufuatia Shirikisho la Soka Tanzania jana kueleza kuwa tarehe ya uchaguzi haitoweza kubadilika na utafanyika kama ulivyopangwa.
Mmoja wa wanachama hao (jina tunalo) amesema haijajulikana kama Yanga inaenda kufanya uchaguzi wa kujaza nafasi za watu watano ama la.
Aidha, ameongoza kuwa wanasubiria kikao cha Kamati ya Uchaguzi kitakachokutana na Baraza la Wadhamini kesho Jumapili ili kufikia mwafaka juu ya namna mchakato huo utakavyokwenda.
Yanga imeamuriwa kufanya uchaguzi huo na Baraza la Michezo nchini (BMT) kufuatia kuwa na uongozi ambao haujakamilika kutokana na baadhi waliokuwepo kuachia ngazi.
0 COMMENTS:
Post a Comment