November 6, 2018


Uongozi wa timu ya Manispaa ya Kinondoni, KMC umesema kuwa bado unaendelea kujiweka sawa kwenye ligi kutokana na kufanikiwa kupata pointi tatu mbele ya Mbeya City katika mchezo uliochezwa jana Uwanja wa Uhuru .

Ofisa habari wa KMC, Anwar Binde amesema kuwa ni mwendelezo mzuri kwao kupata matokeo hasa kwa wakati huu ambao ushindani umekuwa mgumu na kila timu inahitaji matokeo.


"Tulianza taratibu kwa kulazimisha sare na kupoteza baadhi ya michezo ila mwalimu baada ya kugundua makosa ya wachezaji ameweza kuwapa mbinu na taratibu wanazidi kuwa bora, hivyo tunaamini tutaendelea kuleta ushindani siku zote, mashabiki watupe sapoti," alisema.


KMC inapata ushindi wa pili mfululizo baada ya kufanya hivyo kwa Ndanda FC na Mbeya City na michezo yote wakishinda kwa bao moja, wanashika nafasi ya 10 baada ya kucheza michezo 13 wakiwa na point 16.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic