November 6, 2018


Meneja wa zamani wa Arsenal Arsene Wenger yuko karibu kurejea usimamizi huko AC Milan. (France Football - in French)

AC Milan wana mpango wa kumuendea mlinzi wa Manchester United raia wa Ivory Coast Eric Bailly, 24, huku mchezaji huko akikasirishwa na ukosefu wa fursa chini ya umeneja wake Jose Mourinho huko Old Trafford. (ESPN)

Manchester City wanatafuta uwepo wa mshambuliajia wa Lille Nicolas Pepe, 23, huku mchezaji huyo raia wa Ivory akifunga mabao 8 msimu huu. (Manchester Evening News)

Meneja wa Southampton Mark Hughes atafutwa ikiwa Saints watakosa kuwashinda Watford siku ya Jumamosi huku Sam Allardyce na David Moyes wakitarajiwa kuchukua nafasi hiyo. (Mirror)

Mlinzi wa Argentina Pablo Zabaleta, 34, anatarajiwa kuundoka West Ham kuelekea Mashariki ya Kati. (Arab News)


Mshambuliaji wa zamani wa Manchester United striker Zlatan Ibrahimovic, 37 ambaye sasa yuko na LA Galaxy anasema Ligi ya Premier imepewa hadhi ya juu bila sababu. (Four Four Two)

Mchezaji anayelengwa na Manchester United Leroy Sane, 22, anasema yuko upande mji mziuri, wakati wing'a huyo mjerumani akisema ana furaha huko Manchester City. (Evening Standard)

Mshambuliaji wa Senegal na Kasimpasa Mbaye Diagne, 27, analengwa na Wolves mwezi Januari. (Birmingham Mail)


Kipa wa Arsenal na Ujerumani Bernd Leno, 26, anasema hakuna mtu anahisi salama kung'ang'ania jesi nambari moja. (Evening Standard)


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic