November 21, 2018


Wanachama na mashabiki wa Yanga sasa wanapaswa kujiandaa kisaikolojia kuishi maisha bila Yusuf Manji baada ya jina la mwenyekiti huyo kutokuwapo miongoni mwa wagombea 27 waliojitokeza kuwania nafasi mbalimbali katika uchaguzi wa klabu hiyo utakaofanyika Janauri 13, 2019. 

Tofauti na ilivyotarajiwa, Manji hajachukua wala kuchukuliwa fomu kama ambavyo kamati ya Uchaguzi ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) ilitaka Yanga wafanye endapo watahitaji kumrejesha mwenyekiti huyo, badala yake wanachama wanne wamejitokeza kuwania nafasi hiyo. 

Dk Jonas Tiboroha,

Mwanasheria wa TFF, Herman Kidifu aliwataja wagombea waliojitosa kuwania nafasi ya Mwenyekiti ni Dk Jonas Tiboroha, Yono Kevela, Mbaraka Igangula na Erick Ninga. Wanaowania nafasi ya makamu mwenyekiti ni Titus Osoro, Salum Magege Chota na Kevela wakati wajumbe ni Hamad Ally Islamu, Benjamin Jackson Mwakasonda, Sylvester Haule, Salim Seif, Musa Katabaro, Shftu Amri na Said Baraka.

Wengine ni Pindu Luhoyo, Dominick Francis, Seko Jihadhari, Ally Omary Msigwa, Arafat Ally Haji, Geoffrey Boniphace Mwita, Frank Kalokola, Ramadhan Said, Leonard Marango, Bernard Faustin Mabula, Christopha Kashiririka, Athanas Peter Kazige na Faustin Peter Bisangwa.


Mbaraka Igangula

Akizungumza jana, Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Wakili Ally Mchungahela, alisema mchakato wa kuchukua na kurejesha fomu umefungwa rasmi na keshokutwa Ijumaa utafanyika mchujo kwa wagombea wote.


Yono Kevela

“Uchaguzi uko palepale kwa wagombea waliochukua fomu, baada ya mchujo wa Ijumaa kutakuwa na usaili na baadaye wagombea wataingia kwenye kampeni kuelekea katika uchaguzi,” alisema Mchungahela ambaye pia alitoa onyo kwa mtu yeyote atakayejaribu kujipenyeza kuvuruga mchakato wa uchaguzi kwa kuanzisha vurugu, kuwa vyombo vya dola vitafanya kazi yake.

CHANZO: CHAMPIONI

3 COMMENTS:

  1. Najua fika Manji hajaongea kiu chochote na wala haifikirii Yanga ila kuna watu wanapandikiza maneno.

    Protas-Iringa

    ReplyDelete
  2. Kama wanachama wote hawa wamejitokeza tatizo ni nini Yanga uchaguzi usifanyike na Mkuchika wenu?

    ReplyDelete
  3. saleh jembe mpuuz tu,

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic