November 30, 2018


Serikali kupitia Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, imesema itaongeza nguvu kusapoti kazi za wasanii chipukizi ili kuikuza na kuitangaza sanaa kitaifa na kimataifa.


Waziri wa wizara hiyo, Harrison Mwakyembe amesema hayo alipokuwa akizungumza katika Tamasha la Live Stand Up Comedy lililofanyika kwenye Ukumbi wa Lukolo uliopo Tabata Segerea jijini Dar hivi karibuni.

 Mwakyembe, alisema Tanzania kuna vipaji vingi ambavyo vikikuzwa na kupata mafunzo sahihi kuna uwezekano wa kuwa fursa na kutoa ajira kwa wengi hali itakayofanya sanaa iongezeke thamani yake.

"Serikali itahakikisha inafanikisha zoezi la kutoa sapoti kwa wasanii chipukizi hasa katika sekta ambazo wengi hawatambui kama zipo. Mfano wa sanaa ni kama Stand Up Comedy ambazo zimeanza kufanya vizuri na watu wanaipenda.


"Tumepata wadhamini wengi ambao wanashirikiana nasi, hivyo tutakaposaini mikataba na wasanii wengine tutawapa nafasi wasanii wa Stand Up Comedy ambao kazi yao kubwa ni kuelimisha jamii kwa njia ya sanaa," alisema Mwakyembe.


Angel Masaburi 'Chuchudote' ambaye ni mratibu wa tamasha hilo, alisema kuwa anaishukuru Serikali kuwa bega kwa bega na wasanii chipukizi.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic