Beki wa kulia wa timu ya Simba, Shomari Kapombe atalazimika kubakia Afrika Kusini kwa ajili ya matibabu kufuatia majeraha ya kuvunjika mguu aliyoyapata akiwa na timu ya taifa,Taifa Stars nchini Afrika Kusini.
Kapombe aliumia akiwa kwenye kambi ya timu ya Taifa iliyokuwa inajiaanda na kucheza mchezo wa kufuzu Afcon uliopigwa kwenye uwanja wa Setsoto Maseru nchini Lesotho jana na inaelezwa kuwa atakaa nje kwa muda wa miezi mitatu.
Taarifa kutoka ndani ya Simba zimeeleza kuwa beki huyo atalazimika kubakia Afrika Kusini kwa ajli ya kupatiwa matibabu kwa daktari wake maalum kabla ya kurejea nchini kuendelea na majukumu ya timu yake.
Awali uongozi wa shirikisho la soka la Tanzania (TFF) ulipanga kumpeleka nchini Dubai kwa ajili ya kupata matibabu hayo lakini uongozi wa Simba ukapendekeza abakie Afrika Kusini kwa kuwa ana daktari wake maalum.
Kapombe amevunjika mguu karibu na eneo la enka hali ambayo ilisababisha akose mchezo wa jana ambao ulimalzika kwa Stars kufungwa bao 1-0.
POLE SANA KAPOMBE MUNGU AKUPE NAFUU UWEZEKUPONA HARAKA
ReplyDeletepole zake ,ni pigo sana, nafasi yake izibwe kwa umakini na mchezaji aliekamilika kwny ukabaji na kupandsha team!
ReplyDeletePole sana Shomari Kapombe. Kwa uwezo wa Mungu utarajea tena uwanjani kwa nguvu zaidi. Ni pengo kubwa kwa Simba Sports Club na Taifa Stars.
ReplyDeleteDah! walau hata mechi hiyo na Lesotho tungeshinda, lakini ndo hivyo tena. KOCHA KOCHA!
ReplyDeleteDu Mungu akuponye haraka urejee katika majukumu yako!
ReplyDeletekocha wa simba alishawatahadhalisha makocha wa taifa stars kuwafanyisha mazoezi magumu lakini hawasikii wakati ule tuliona kina mkude walipata majeraha sasa hivi Kapombe
ReplyDelete