November 19, 2018


Mshambuliaji wa Simba, Adam Salamba, yupo mbioni kutimkia kwenye Klabu ya Royal Sporting Club Anderlecht inayoshiriki Ligi Kuu ya Ubelgiji.

Mshambuliaji huyo mwenye mabao mawili katika ligi ya msimu huu, aliyejiunga Simba akitokea Lipuli msimu huu, amepata nafasi hiyo kutoka kwa wakala wa beki wa Rayon Sport, Abdul Rwatubyaye anayeishi nchini humo.

Taarifa za uhakika kutoka ndani ya Simba, zinasema mchezaji huyo anatarajia kuondoka nchini Desemba, mwaka huu kwa ajili ya kufanya majaribio ya wiki moja kwenye timu hiyo inayokamata nafasi ya nne, mbele ya vinara wa ligi hiyo, KRC Genk anayoichezea Mbwana Samatta.

“Salamba anaweza kuondoka mwezi ujao kuelekea Ubelgiji kwenda Anderlecht kwa ajili ya kufanya majaribio ya wiki moja, kuna wakala wa huko ndiyo anafanya hiyo mipango ya kumpeleka baada ya kuvutiwa na uwezo wake kwani ameanza kumfuatilia tangu akiwa na Lipuli.

“Mipango ndiyo ipo kwenye mchakato wa kuweza kuona mambo yanakwenda vipi ila huyo wakala ndiye anajua kila jambo na mambo ya safari ingawa inafahamika kama atakaa huko kwa wiki moja katika majaribio yake,” alisema mtoa taarifa.

Championi Jumatatu lilimtafuta Mwenyekiti wa Simba, Swedy Mkwabi, akasema: “Bado sijapata taarifa za mchezaji huyo, hayo masuala ya timu yote yanajadiliwa kwanza na C.E.O ambaye ni (Crescentius) Magori pamoja na kocha kabla ya baadaye bodi kukutana na kujadiliana.”

Magori alipotafutwa jana, simu yake ya mkononi haikupokelewa.

2 COMMENTS:

  1. kama Mkwabi ndivyo alivyojibu, ni vizuri na waandishi wakabadili weledi na nani wa kumuuliza kitu gani! kila kiongozi ana maswali yake jamani !

    ReplyDelete
  2. Mpira una njia zake,na ili mchezaji wa kitanzania acheze kwa mafanikio lazima azifuate hizo njia,kitu kisichowezekana kwa kizazi cha sasa kitoke bongo na moja kwa moja aende ulaya kucheza ligi kuu kubwa na acheze kwa mafanikio ni ndoto ya mchana hiyo,Simkatishi tamaa ila inabidi afuate njia kwanza acheze timu kubwa za either afrika kaskazini,Kusini au magharibi na afanye vizuri then ataenda Ulaya hapo atafanikiwa ila kama anataka kwenda kutembea tu aende

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic