November 27, 2018


Imeelezwa kuwa mabosi wa Yanga wameanza mazungumzo ya kimyakimya na beki wa Liipuli FC, Ally Sonso ambaye yupo katika kikosi cha Taifa Stars.

Beki huyo ambaye ni tegemeo ndani ya kikosi cha Lipuli, ameingia katika rada za Yanga ikiwa mpaka sasa dirisha dogo la usajili likiwa wazi.

Licha ya tetesi za kumsajili beki huyo kushika kasi, viongozi wa Yanga wameshindwa kuliweka wazi, pengine wanataka kufanya kwa staili ya kimyakimya.

Taarifa za ndani kutoka Yanga zinasema kuwa Kocha Mkuu, Mkongomani, Mwinyi Zahera, ndiye aliyependekeza jina la mchezaji huyo kutua Yanga.

Wakati huo kikosi cha Yanga baada ya kumalizana na Kagera Sugar juzi kwa kuitandika mabao 2-1 huko Kaitaba, kikosi hicho kitawasili leo Dar es Salaam kuendelea na safari ya mechi zijazo za ligi.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic