November 13, 2018










Mbabane Swallows ya Swazilland  ambao ni waoinzani wa Simba katika mashindano ya Ligi ya Mabingwa Afrika, Simba wameshtuka na kuamua kujipima na Big Bullets kutoka Malawi siku ya Ijumaa.
Swallows wanatambua juu ya nyota wakali wa Simba wakiongozwa na Meddie Kagere pamoja na Okwi kupachika mabao watamenyana na Simba Dar es Salaam kati ya Novemba 27-28.

Imeelezwa kuwa kocha Mkuu wa Simba Patrick Aussems ndiye amechagua timu hiyo ili kuweza kuwaweka sawa wachezaji wake kimataifa.

"Alianza kwa kucheza mchezo wa kirafiki dhidi ya Azam ambapo tulifanikiwa kushinda bao 1-0 hivyo ili kuendele kuwa imara zaidi tutacheza na timu kuoka Zambia," alisema. 

 Simba wanaingia kwenye mechi za kimataifa baada ya kupita zaidi ya miaka mitano bila kushiriki wakiwa wameboresha kikosi chake hasa kwa kuwa na wachezaji wenye uzoefu na mechi za kimataifa.

3 COMMENTS:

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic