November 13, 2018

Mwenyekiti wa kamati ya Uchaguzi ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) Malangwe Mkuchukia, amesema kuwa zoezi la Uchaguzi wa Yanga linaendelea kama ilivyopangwa.

Mkuchika amesema kwamba licha ya viongozi wa Baraza la wadhamini wa klabu ya Yanga kutoa tamko la kuendelea kumtambua Yusuphu Manji kuwa ndiye Mwenyekiti lakini kwao sio kigezo cha kutoendelea na Uchaguzi.

"Kama wanamtaka Manji awe kiongozi wao basi inabidi afuate utaratibu achukue fomu ama wamchukulie ili agombee, hatupo tayari kuona viongozi ama wanachama wanataka kuuingilia uchaguzi hatutakaa tukawachekea tutawashughulikia wote, wasipite mlango wa uani," alisema.

Uchaguzi wa Yanga unatarajiwa kufanyika Januari 13 kwa ajili ya kuziba nafasi ambazo ziliachwa wazi ikiwa ni pamoja na ya mwenyekiti Yusuphu Manji ambaye aliandika barua ya kujiuzulu tangu  mwezi Mei mwaka jana.

3 COMMENTS:

  1. HAHAHA FYEKELEA MBALI WOTE LAZMA WAFANYE UCHAGUZI MTANI MBONA UNAGOMA KUFANYA UCHAGUZI KWAN SHDA IKO WAPI KAMA MANJI AMERUDI BASI MCHUKULIE / ACHUKUE FORM ILI MAMBO YAWE SAWA

    ReplyDelete
  2. Hakuna sababu ya kuendeleza migogoro isiyo na tija. Watumie busara kwa kuwaita viongozi (baraza la wadhamini)wawaambie kuwa nafasi zote zitagombewa kuliko kuweka kila kitu kwenye media. Yanga ina watu watulivu watamchukulia fomu mwenyekiti au atachukua mwenyewe na atapita

    ReplyDelete
  3. Wanataka kupiga hela tu wasenge hawa fomu wangekua wanagawa bure wangemlazimisha kwel achukue?

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic