Kamati ya Maadili ya Shirikisho la Mpira Tanzania (TFF) iliyo chini ya Mwenyekiti Hamid Zembwezeleni imemfungia Mwenyekiti wa matawi ya Yanga Bakili Mohamed na Katibu wake Boaz Kupilika kutojihusha na masuala ya soka kwa kipindi cha miaka 3.
Mbali na adhabu hiyo pia wanatakiwa kulipa faini ya shilingi Milioni 2 kila mmoja kwa kukaidi maamuzi ya Serikali na TFF yanayohusiana na maagizo ya kufanyika Uchaguzi wa kujaza nafasi ambazo ziko wazi ndani ya klabu ya Yanga.
Hivi karibuni Serikali na TFF ilitoa maagizo kwa Yanga kufanya uchaguzi wa kuziba nafasi zilizo wazi ikiwa ni pamoja na ya Mwenyekiti Yusuphu Manji aliyejiuzulu zoezi ambalo limekuwa likisuasua kutokana na baadhi ya viongozi kuzuia wanachama kuchukua fomu kwa kudai kuwa Manji bado ni kiongozi.
HIYO TFF NI TAWI LA SIMBA ILA KITAELEWEKA TU,
ReplyDeleteMawazo mgando ndugu zangu wanajangwani. Tufanye uchaguzi ili tuongozwe na viongozi kwa mujibu wa Katiba ya Yanga inavyotaka. Mashabiki wa Yanga tutaonekana hatuna akili kwa kuendelea kuamini tunaongozwa na kivuli cha mwenyekiti aliyejiuzuru.
Delete