November 26, 2018


Msemaji wa Klabu ya Simba, Haji Manara amefunguka kuhusu maandalizi ya mechi yao ya Kimataifa dhidi ya Mbabane Swallows FC ya nchini Swaziland, na kudai kuwa wamepokea taarifa kutoka TTF tayari kwa mchezo huo unaotarajiwa kutimua vumbi keshokutwa November 28 , 2018 katika Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Akizungumza na vyombo vya habari jijini Dar es salaam leo, Manara amesema; “Tunakwenda kuwakabili Mbambane keshokutwa Jumatano tukijua ni timu nzuri na mabingwa wenzetu, lakini tunajua matarajio ya watanzania na wanasimba kwetu,kiukweli hatutawaangusha na tunaahidi furaha kwenu.

Viingilio ni ;

5,000
7,000
10,000 
20,000

‘Tukutane Uwanja wa Taifa Saa kumi alasiri Tarehe 28/11/2018 ,Tunawaomba Watanzania na Wanasimba tuujaze uwanja na kuwapa nguvu wachezaji wetu.”

Mbabane Swallows FC tayari wamemewasili nchini leo usiku huku akijinasibu kuwa wamejipanga vyema kuikabili timu hiyo.

1 COMMENTS:

  1. Kwa mfano hii mechi ingepigwa saa nane kuna tatizo kwa wachezaji wetu???mi naamini kutokana na mfumo wa Kijiografia tungeweza kuifanya hii mechi icheze mapema zaidi kuliko huo muda. Naamini tatizo letu ni maandalizi pia kwa wachezaji wetu kuhimili huo muda. Tujaribu kuzingatia matokeo zaidi kwenye hizi mechi kuliko kujaza watu uwanjani maana matokeo ndio yatatupa faida zaidi.
    Hata mechi ya Uganda na Tanzania pia ingechezwa muda huo huo pia

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic