November 28, 2018


Na George Mganga

Baada ya kuadhibu vikali Northern Dynamo ya huko Ushelisheli kwa mabao 4-0 katika mchezo wa kwanza wa Kombe la Shirikisho Afrika, uongozi wa klabu ya Mtibwa Sugar umewaombea ushindi Simba leo.

Mtibwa wameitwanga Dynamo ambapo mechi imepigwa kwenye Uwanja wa Azam Complex uliopo pembezoni kidogo mwa jiji la Dar es Salaam na kuanza kuipeperusha vema bendera ya taifa la Tanzania.

Kwa mujibu wa Msemaji wa Mtibwa, Thobias Kifaru, amesema leo itakuwa ni zamu ya Simba kuendeleza dozi ili kuliweka jina la Tanzania katika ramani nzuri ya soka na kulitangaza vizuri kimpira.

Kifaru anaamini Simba itafanya vema pia kulingana na namna maandalizi waliyoyafanya kuelekea mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika watakapocheza na Mbabane Swallows ya Swazilland majira ya saa 10 kamili jioni.

"Tumefurahia matokea ya leo (jana), sasa ni zamu ya Simba kucheza karata yao ya kwanza kwenye ligi ya mabingwa Afrika dhidi ya Mbabane, tunawaombea wafanye vizuri ili kuzidi kuipeperusha bendera ya taifa letu la Tanzania" alisema.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic