November 28, 2018


Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) limesema mchezo wa Ligi Kuu Bara ambao JKT Tanzania Februari 19 2019 watakuwa wenyeji dhidi ya Yanga utapigwa katika Uwanja wa CCM Mkwakwani, Tanga.

Kwa mujibu wa Ofisa Habari wa TFF, Clifford Mario Ndimbo, ameeleza kuwa mechi hiyo ni lazima ichezewe Mkwakwani kwani JKT Tanzania ndiyo wanautumia kwa mechi za nyumbani.

Ufafanuzi wa TFF umetolewa kutokana na klabu hiyo kutuma maombi ikiomba mechi hiyo isichezewe Dar es Salaam baada ya kudhania ingepigwa jijini humo sababu mchezo utakuwa ni wa kiporo.

Ndimbo amewaambia JKT Tanzania kutokuwa na wasiwasi kwani ni haki yao kuchezea Mkwakwani kwa sababu wameuchagua kuwa uwanja wao wa nyumbani.

Ikumbukwe pia Simba walienda kuchezea Mkwakwani katika mechi na JKT na kufanikiwa kuibuka na ushindi wa mabao 2-0.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic