November 27, 2018


Inawezekana kabisa wekundu wa Msimbazi, Simba SC, wanaweza wakawa wametibuliwa mipango yao ya kumsajili kiungo wa Gor Mahia FC, Francis Kahata.

Taarifa ambazo bado ni za moto zinasema Kahata yuko kwenye hatua za mwisho kumalizana na USM Alger ya Algeria ambayo imeonesha nia ya kupata msaada wake.

Kahata ameanza kuhusishwa kusajiliwa na Simba kwa miezi kadhaa lakini hakuna mpaka sasa hakuna chochote kinachoendelea juu ya timu hiyo na Kahata.

Kiungo Kahata amekuwa kwenye fomu na tegemeo ndani ya Gor Mahia na timu nyingi haswa ukanda wa Afrika zimekuwa zikimuwania ili zimsajili.

Bado mpaka sasa dili hilo halijakamilika kati yake na USM Alger, hivyo tuendelee kusubiria ili kujua hatma yake na Gor Mahia pamoja na kutua Simba pia.

5 COMMENTS:

  1. Pia Francis Kahata anahusishwa kuhamia Black Leopards ya Afrika Kusini ambayo inafundishwa sasa na Darren Kerry ambae ni kocha wake wa zamani wa Gor Mahia

    ReplyDelete
  2. Acheni kukuza mambo mnampigia chapuo kahata aje simba.simba ina management kubwa inayowweza kusajiri kutokana na matakwa ya kocha na si kusajir kwa magazeti.huyo kahata ni mchezaji wa kawaida mno kwa simba alikuwepo tangu kitambo gor

    ReplyDelete
  3. Acha aende kwanza simba tuna viungo washambuliaji wengi tu

    ReplyDelete
  4. Sizitaki mbichi hizi""mlikuwa mnamtaka sana Kahata.
    Mlisajili Chama wakati mnajua kuna Niyo pia mkamuongeza Dilunga.

    ReplyDelete
  5. Simba ina uwezo wa kumsajili mchezaji yeyote Afrika. Lakini haifanyi hivyo kiholela. Kocha amesema anataka mshambuliaji anayejua kufunga kuliko Okwi na MK14, na mwenye uwezo wa kucheza pia kama kiungo. Francis Kahata hana sifa hizo! Pia anataka beki wa pembeni anayepia miguu yote miwili, na awe na sifa ya ziada ya kucheza kama beki wa kati. Hao ndio wachezaji wanaotakiwa na Simba. Acheni kuleta stori za ajabu ajabu.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic