November 27, 2018


Na George Mganga

Uongozi wa klabu ya Simba umesema ujio wa wachezaji wake wawili, Emmanuel Okwi na Juuko Murushid utawapa nguvu kwenye mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Mbabane Swallows.

Kwa mujibu wa Ofisa Habari wa klabu, Haji Manara, amesema kurejea kwa Okwi na Murushid kutasaidia kukiweka kikosi katima hali nzuri ili kupigania ushindi kwenye kipute hicho cha kimataifa.

Wawili hao walikuwa kwao Uganda kwa ajili ya majukumu ya timu ya taifa ambapo walikuwa na kibarua dhidi ya Cape Verde kuelekea kuelekea michuano ya AFCON mwakani huko Cameroon.

"Wachezaji wetu Emmanuel Okwi na Juuko Murushid tayari wamesharejea, kwa namna moja ama nyingine watakuwa wanaongeza nguvu na ari kuelekea mechi yetu ya Ligi ya Mabingwa Afrika na Mbabane" alisema.

Tayari Okwi na Murushid wamesharejea na wameanza mazoezi kuelekea mechi na Mbabane ambayo itachezwa kesho Jumatano majira ya saa 10 jioni kwenye Uwanja wa Taifa Dar es Salaam.


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic