November 28, 2018


Kutokana na uongozi wa klabu ya JKT Tanzania kutaka mechi yao dhidi ya Yanga ipigwe uwanja wa CCM Mkwakwani, Tanga, imebainika kuwa wanataka kupata faida ya mapato kama wenyeji.

Siku mbili zilizopita JKT Tanzania walituma barua kwenda TFF wakiomba mechi yao na Yanga ichezewe Tanga kutokana na Uwanja wa mechi zao za nyumbani upo mjini humo.

Taarifa zinasema JKT Tanzania wamekuwa wajanja na wanachokihitaji kwa sasa ni kupata fedha za mapato yanayotokana na viingilio vya watazamaji.

Ikumbukwe sheria ya mapato hivi sasa imekuwa tofauti na ile ya msimu uliopita na sasa yote yanakuwa yanaenda kwa mwenyeji na mgeni haambulii chochote.

Tayari TFF imeshwaambia JKT Tanzania mechi hiyo ambayo itapigwa Februari 9 mwakani itachezewa CCM Mkwakwani kwa sababu walishauchagua uwanja huo kuchezea mechi za nyumbani.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic