November 28, 2018


Baada ya kuenea kwa tetesi kuwa uongozi wa Yanga upo kwenye mazungumzo na beki tegemo wa Lipuli, Ally Sonso kwa ajili ya kumsajili, mabosi wa mchezaji huyo wamesema hawana taarifa yoyote.

Lipuli wamwefunguka kuwa hawajapokea simu yoyote kutoka Yanga ikieleza kumtaka Sonso ambaye ameitwa kwenye kikosi cha timu ya taifa 'Taifa Stars' na Kocha, Emmanuel Amunike.

Uongozi umesema kama wangekuwa wameshaanza mazungumzo na Yanga wasingekuwa na haja ya kuficha bali walngeliweka wazi ili kila shabiki na mdau wa mpira afahamu.

Licha ya kusema hawajapokea simu kutoka Yanga, taarifa zinasema Lipuli wao hawana shida kwa Sonso kuelekea Yanga, ni fedha yao tu kama watakubaliana dau.

Taarifa hiyo imesema Lipuli wameeleza kuwa mpira ni biashara hivyo kama Yanga wamejipanga vizuri ni vema wakaenda kukaa nao mezani wafikie mwafaka.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic