November 12, 2018



Kikosi cha timu ya Taifa ambacho kinaendelea na maandalizi yake ya mchezo dhidi ya Lesotho wa kuitafuta tiketi ya kufuzu kushiriki mashindano ya Ligi ya Mataifa ya Afrika (Afcon) mwakani Cameroon kimeendelea kuongezewa nguvu baada ya wachezaji wanaocheza nje kuanza kuripoti leo.

Meneja wa Taifa Stars, Dany Msangi amesema kuwa wachezaji Ramadhan Kessy (Nkana, Zambia), Rashid Mandawa (BDF, Botswana) na Abdi Banda (Baroka, Afrika Kusini), Kimid Mao (Petrojet, Misri) anatarajiwa kuripoti leo.

 Golikipa Beno Kakolanya na mshambuliaji Yahya Zayd  wamekuwa ni sehemu ya kikosi ambacho kimefanya mazoezi leo katika uwanja wa Celtic Bloemfontein.

Mchezo huo wa kundi L utachezwa Novemba 18, 2018 Maseru, Lesotho ukiwa ni wa marudio baada ule wa awali uliochezwa Tanzania kumalizika kwa sare.


 

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic