November 13, 2018



Imeelezwa kuwa wajumbe wa muwekezaji, Mohamed Dewji 'Mo' wamepatikana ili kuunda bodi ya wakurugenzi wa Simba, wakurugenzi hao wataungana na wajumbe  waliochaguliwa na wanachama ili kuunda rasmi bodi ya wakurugenzi ndani ya klabu ya Simba kutokana na mabadiliko ya uendeshaji.

Wajumbe walioteuliwa kwa upande wa Mohamed Dewji, 'Mo' ni pamoja na Mohamed Nassoro, Hans Poppe, Prof. Mohamed Janabi, Musleh Al Rawahi, Barbara Gonzalez na Octavian Mshiu.

Katiba ya Simba inampa nafasi Mwenyekiti Sued Mkwabi kuteua wajumbe, amewateua Hassan Kapusi na Salim Abdallah 'Try again' ambaye aliwahi kuwa kaimu nafasi ya Rais na aliacha kugombeaa baada ya kusema kuwa amewaachia wengine kupata nafasi.

Wajumbe wapya walioteuliwa ni pamoja na Asha Baraka, Dr Zawad,Hussen Kitita,Seleman Harub na Mwina Kaduguda.

1 COMMENTS:

  1. Safu nzito sana hii, ipelekeni mbaaali Simba iwe mfano wa Kuigwa Tza, kila lenye kheri kwenu, cc tunasubiri kununua HISA

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic