November 6, 2018


Na George Mganga

Kundi la Waadilifu wa Simba limekabidhi zawadi ya katoni 60 za maji ya kunywa kwa timu ya Simba chini ya miaka 20.

Kundi limeamua kutoa msaada huo kama hamasa kwa timu hiyo ambayo ni tegemeo hapo baadaye katika timu ya wakubwa na Taifa Stars kwa ujumla.

Licha ya kutoa katoni hizo, uongozi wa kundi kupitia kwa Mwenyekiti wake, Johansen Karwani, umesema ni vema matawi mengine yakawaiga ili kutekeleza adhma ya kauli mbiu yao ijulikanayo kama Simba Nguvu Moja.

Waadilifu wa Simba limekuwa ni kundi lenye kujitoa kuzisaidia timu zao kila mara kwa ajili ya kuamsha morali kwa wachezaji wazidi kujituma.

Hii si mara ya kwanza bali imekuwa ni mwendelezo wa kundi hilo kufanya hivyo.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic