November 7, 2018


Imeelezwa kuwa wachezaji wanne wa klabu ya Yanga jana wameshindwa kufika mazoezini katika Uwanja wa Chuo cha Polisi kilichopo maeneo ya Kurasini, Dar es Salaam.

Wachezaji hao ambao ni Ibrahim Ajibu, Matheo Anthony, Mrisho Ngassa na Andrew Vincent hawakuweza kufika huku ikielezwa hawakutoa taarifa kwa uongozi.

Haijajulikana sababu za wachezaji hao kushindwa kuwasili mazoezini jana ambapo kikosi cha Yanga kinajiandaa na mechi zijazo za Ligi Kuu Bara.

Licha ya kushindwa kuwasili suala la kipindi cha mpito Yanga linahusishwa juu ya wachezaji hao kutofika mazoezini.

Katika mchezo wa mwishi uliopita Yanga ililazimishwa sare ya bao 1-1 na Ndanda FC ya mjini Mtwara kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

1 COMMENTS:

  1. Et kipindi cha mpito acha kuficha siri,akina ajibu walikua wanacheza wakijua manji ararudi nyumbani hatimae manji ndio hivyo tena sasa wanahofia ugali wao wataupata vp,msizunguke waelezeni wachezaji ukweli.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic