November 2, 2018


Manchester City walifanikiwa kuwalaza Fulham 2-0 kwenye mechi ya Kombe la Ligi iliyochezwa Alhamisi lakini wameingiwa na wasiwasi kuhusu kiungo wao nyota Kevin de Bruyne.

De Bruyne alichechemea na kuondoka uwanjani baada ya kuonekana kuumia dakika tatu kabla ya mechi kumalizika.

kwa mujibu wa BBC, Nyota wa mechi hiyo alikuwa kinda Mhispania Brahim Diaz ambaye alifunga bao moja kila kipindi, dakika ya 18 na 65, hayo yakiwa mabao yake ya kwanza kufungia timu kubwa ya Manchester City.

City sasa watakutana na mshindi wa mechi kati ya Leicester na Southampton kwenye hatua ya robo fainali ya michuano hiyo ambayo hufahamika kama Kombe la Carabao.

Mbelgiji De Bruyne mwenye miaka 27 alikuwa ameanza mechi kwa mara yake ya pili pekee msimu huu tangu alipopata jeraha kwenye kano za goti lake la kulia mwezi Agosti.

"Anachunguzwa na madaktari," alisema meneja wa City Pep Guardiola baada ya mechi.

"Hatujafahamu kufikia sasa iwapo hakuna kitu chochote kibaya kimemtendekea au kama ni kitu kibaya."

De Bruyne alikuwa amecheza vyema sana na kuonekana kujituma uwanjani lakini aliondoka uwanjani akiwa anagusa goti lake la kushoto, na moja kwa moja akaelekea chumbani kupokea matibabu.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic