November 21, 2018


Wakati kikosi cha Yanga kikiwa mjini Shinyanga tayari kujiandaa na mecho wa kesho Alhamisi dhidi ya Mwadui FC, wachezaji wawili wa timu wamegoma kusaifiri kuelekea mkoani humo kwa madai ya kutolipwa stahiki zao, imeelezwa.

Wachezaji hao ambao walipaswa kuondoka leo baada ya kuwasili nchini wakitokea Lesotho kuitumikia Taifa Stars, ni beki Kelvin Yondani pamoja na kipa namba moja ambaye pia ni tegemeo ndani ya kikosi, Beno Kakolanya.

Inaelezwa kuwa Yondani na Kakolanya hawajalipwa fedha za mishahara wa miezi minne pamoja na zile za usajili jambo ambalo limesababisha wagome kusaifiri.

Yanga imeanza mazoezi leo kujiweka fiti kuelekea mchezo wa kesho utakaopigwa kwenye Uwanja wa CCM Kambarage, Shinyanga majira ya saa 10 kamili za jioni.

Aidha, Yanga itawakosa wachezaji wake baadhi ikiwemo Papy Tshishimbi na Juma Mahadhi ambao bado mpaka sasa wapo majeruhi.

8 COMMENTS:

  1. wanatafuta wachezaji wapya huku hawajamaliza na waliopo

    ReplyDelete
  2. Sasa siwanasema manji bado mwenyekiti bas awalipe

    ReplyDelete
  3. Hao wamebaki dar ili kukutana na viongozi wa timu fulani waweze kusaini kwenye hili dirisha dogo. Habari za kuthibitika kutoka kwa mtu wa karibu wa Kevin Yondani amesema wanadai mishahara ya muda mrefu na kutokana na kanuni za kimkataba Yanga wamevunja mkataba wa wachezaji hao kwa kutolipa mishara kwa zaidi ya Miezi mitatu. Kiongozi huyo wa klabu hiyo amesema wakiafikiana huenda wakatangazwa ndani ya siku mbili kama wachezaji wao kamili. Tusubili tuone itakavyokuwa. Muda huu ninavyoandika Kiongozi huyo pamoja na Wachezaji hao wamo kwenye Hotel Maarufu katikati ya Jiji kwa mazungumzo ya kimaslahi.

    ReplyDelete
  4. He sasa majembe hayo yakiondoka itakuwaje?

    ReplyDelete
  5. Ikiwapendeza waende tu ila yanga ipo tangu 193...huko hivyo itapata mbadala wao tu...hiki ni kipindi cha mpito tu

    ReplyDelete
  6. Habari nyingi za kitanzania no za udakuzi yaani hazifanyiwi uchambuzi yakinifu. Mwandishi nae anapita sehemu anayoamin itawachukua akili. Kelvin Yondan gharama zake za usajil zilisimamiwa na abasi Tarimba chini ya watoa pesa tawi Viva la Mwanza. Kakolanya bado alikuwa ndani ya mkataba. Hata kocha mkuu hakusafir na timu juz ameondoka jana

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic