November 21, 2018


Kocha Mkuu wa Yanga, Mwinyi Zahera, amesema pamoja na kikosi chake kuwa na matatizo kadhaa, anaamini kitapambana kuhakikisha kinapata pointi 3 dhidi ya Mwadui FC, kesho.

Kauli ya Zahera imekuja kufuatia Yanga kukumbukwa na changamoto za kuyumba kiuchumi hiki ikielezwa baadhi ya wachezaji wamegoma kusafiri na timu.

Zahera anaamini Yanga itaweza kupata matokeo kutokana na wachezaji ilionao na namna ambavyo imejiandaa.

Yanga itakuwa inacheza mechi yake ya kwanza kesho ikiwa nje ya Dar es Salaam kwa msimu kwenye Uwanja wa CCM Kambarage, Shinyanga.

Kuelekea mechi hiyo Yanga itawakosa wachezaji wake kadhaa ikiwemo Juma Mahadhi ambaye ni majeruhi.

1 COMMENTS:

  1. Jamani tutafuteni fedha tuwalipe hawa watu ili timu iendelea kufanya vizuri..

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic