Kikosi cha timu ya Yanga kimeanza kibabe mchezo wao wa kwanza wa leo nje ya Dar es Salaam kwa ushindi wa bao 2-1 dhidi ya Mwadui FC katika mchezo uliochezwa uwanja wa CCM Kambarage.
Yanga wamefanikiwa kuendeleza rekodi yao kwa kucheza michezo 11 bila kupoteza na kwa matokeo hayo wamefikisha pointi 29 na kuishusha Simba nafasi ya pili kwenye msimamo wa Ligi Kuu, wakiwa wameachwa pointi moja na Azam FC wenye pointi 30.
Mabao ya Yanga yamefungwa na mshambuliaji Herieter Makambo na Mrisho Ngasa akifunga bao la pili la ushindi.
Yanga wamecheza leo bila ya kuwa na wachezaji wao kama Ibrahim Ajibu, Kelvin Yondani, Beno Kakolanya na Papy Tshishimbi.








Kwa ubabe gani sasa?yanga hakuna mpira ni kama man u wanaotea magoli tu ila kiuhalisia hakuna kitu pale,ngoja wasubirie mziki wa azam,coastal,jkt,simba ndio utapata majibu.
ReplyDeleteKwani coastal union hawajacheza na yanga? Au hawajacheza na simba s.c?
DeleteKuna mbao na Ndanda nimezisahau,kama umesuluhishwa kwenu,away unapigwa tu huna namna.
ReplyDeleteKuna mbao na Ndanda nimezisahau,kama umesuluhishwa kwenu,away unapigwa tu huna namna.
ReplyDeleteTumeanza na mwadui nje ya dar
DeletePovuuuu iloo mhhh
ReplyDeleteWalisema yanga akitoka nje ya Dar ni kichapo tu!! Sasa wamepata ushindi wanasema ngojea simba na azam !!!
ReplyDeleteSimba si walishindwa pia kupata ushindi waliokuja nao mfukoni?? Mpira unadunda bro!!
Walikuwa wanasema ngoja mtoke nje ya Dar,tumetoka nje ya Dar tumeanza na ushindi wamebadili kibao eti ngoja Simba na Azam wanasahau Simba tumeshacheza nao mechi imeisha draw haha wamechanganyikiwa,mechi ya pili tunawapiga Simba na ubingwa huooooooo unarudi ulikozoea
ReplyDeleteMashabiki Wa simba huwa wana maneno mengi xna na ngoja ngoja nyingi .......zidishen maombi yenu mabaya mzid kuumbuka hamna lolote mikia FC
ReplyDeletemasikini wa hela sisi wanajangwani lakin uwanjan mabilionea.
ReplyDelete