November 22, 2018


Kikosi cha timu ya Yanga kimeanza kibabe mchezo wao wa kwanza wa leo nje ya Dar es Salaam kwa ushindi wa bao 2-1 dhidi ya Mwadui FC katika mchezo uliochezwa uwanja wa CCM Kambarage.

Yanga wamefanikiwa kuendeleza rekodi yao kwa kucheza michezo 11 bila kupoteza na kwa matokeo hayo wamefikisha pointi 29 na kuishusha Simba nafasi ya pili kwenye msimamo wa Ligi Kuu, wakiwa wameachwa pointi moja na Azam FC wenye pointi 30.

Mabao ya Yanga yamefungwa na mshambuliaji Herieter Makambo na Mrisho Ngasa akifunga bao la pili la ushindi.

Yanga wamecheza leo bila ya kuwa na wachezaji wao kama Ibrahim Ajibu, Kelvin Yondani, Beno Kakolanya na Papy Tshishimbi.

10 COMMENTS:

  1. Kwa ubabe gani sasa?yanga hakuna mpira ni kama man u wanaotea magoli tu ila kiuhalisia hakuna kitu pale,ngoja wasubirie mziki wa azam,coastal,jkt,simba ndio utapata majibu.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Kwani coastal union hawajacheza na yanga? Au hawajacheza na simba s.c?

      Delete
  2. Kuna mbao na Ndanda nimezisahau,kama umesuluhishwa kwenu,away unapigwa tu huna namna.

    ReplyDelete
  3. Kuna mbao na Ndanda nimezisahau,kama umesuluhishwa kwenu,away unapigwa tu huna namna.

    ReplyDelete
  4. Walisema yanga akitoka nje ya Dar ni kichapo tu!! Sasa wamepata ushindi wanasema ngojea simba na azam !!!
    Simba si walishindwa pia kupata ushindi waliokuja nao mfukoni?? Mpira unadunda bro!!

    ReplyDelete
  5. Walikuwa wanasema ngoja mtoke nje ya Dar,tumetoka nje ya Dar tumeanza na ushindi wamebadili kibao eti ngoja Simba na Azam wanasahau Simba tumeshacheza nao mechi imeisha draw haha wamechanganyikiwa,mechi ya pili tunawapiga Simba na ubingwa huooooooo unarudi ulikozoea

    ReplyDelete
  6. Mashabiki Wa simba huwa wana maneno mengi xna na ngoja ngoja nyingi .......zidishen maombi yenu mabaya mzid kuumbuka hamna lolote mikia FC

    ReplyDelete
  7. masikini wa hela sisi wanajangwani lakin uwanjan mabilionea.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic