November 20, 2018


Mratibu wa Yanga, Hafidhi Saleh amesema kuwa kikosi kipo tayari kwa ajili ya kuwavaa Mwadui kutokana na uwezo wa kupata matokeo na maandalizi ambayo wameyafanya.




Yanga wamefanikiwa kuanza mzuguko wa kwanza vizuri kwani katika michezo 10 ambayo wamecheza wameshinda michezo 8 na kutoa sare michezo 2 na kukusanya pointi 26.

"Tumejiandaa kiasi cha kutosha kuhakikisha tunapata matokeo nje ya Dar, mashabiki waendelee kutupa sapoti, wachezaji wapo vizuri na wana morali kubwa katika mchezo wetu dhidi ya Mwadui FC," alisema.


Mchezo huo utachezwa Novemba 22 uwanja wa Kambarage Mkoani Shinyanga ukiwa ni mchezo wa kwanza nje ya Dar es Salaam baada ya kucheza michezo 10 yote  uwanja wa Taifa.

1 COMMENTS:

  1. Kuna mtandao umesukwa kutokea Serikalini, Wizarani, Magazeti, waandishi wa Habari, BMT na TFF, Body ya Ligi na baadhi ya wanachama maarufu wa Yanga, kwa lengo la KUIHUJUMU NA KUIDHOOFISHA YANGA....mfano Uchaguzi angalia mchakato mzima....kabla, na wakati wa uchaguzi wenyewe. Angalia kwenye mechi ya kirafiki Namungo njoo kwenye wachezaji wa Timu za Taifa (u23 na Taifa Stars) hawajaripoti kambi ya Yanga kwenda kucheza mechi na mwadui...Bodi ya Ligi ingesogeza mechi yao ili kuruhusu wachezaji wao wajiunge na timu hawakufanya hivyo....ila Simba wameruhusiwa. Ukija kwenye mchakato wa ratiba za mechi zilizopangwa na bodi ya ligi....njoo uangalie sarakasi za uchaguzi...Swali Kwanini kakolanya, Yondani, ninja, kabwili na Paulo Godfrey hawatajiunga na Timu ili kuwahi mechi na Mwadui. Wenye akili tushajua hili...

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic