Baada ya Baraza la Michezo Tanzania (BMT) na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kuitaka Yanga kuitisha uchaguzi wake kwa ajili ya kujaza nafasi zilizo wazi ikiwemo ya Manji aliyeandika barua ya kujiuzulu Mei 2017 baraza la wadhamini limetoa tamko.
Mwenyekiti wa Baraza la wadhamini wa Yanga ambaye ni Waziri wa Nchi,Ofisi ya Rais, Utumishi wa Umma na Utawala Bora, George Mkuchika amesema kuwa Mwenyekiti wa Yanga, Yusuphu Manji amerejea rasmi.
"Ameandika barua ya kukubali ombi la wanachama wa klabu baada ya kukataa kujiuzulu kwakwe, hivyo baraza la wadhamini linamtambua Manji kama Mwenyekiti na hatutakwenda kinyume na matakwa ya wanachama.
"Mwenyekiti karudi, Manji amerudi ametuma barua yake sasa kama amerudi yeye ndiye kiongozi wetu amesharudi na Lingalangala yeye ni kaimu Mwenyekiti," alisema.
Uchaguzi wa Yanga ulipangwa kufanyika tarehe 13 januari mwakani na fomu zilitangazwa kutolewa TFF na Ofisi ya Yanga.







Kauli ipi tuiamini ya mh.Mwakyembe Waziri wa michezo au mh Mkuchika Mwenyekiti wa baraza la wadhamini juu ya Mwenyekiti wa Yanga wote wametoa kauli siku moja zikipingana.
ReplyDeleteYanga kuweni makini kwani ikiwa TFF na Kamati zake zote hazitakuwa zimepata copy ya barua ya Kaman Manji amerejea....na wakaendelea na uchaguzi...italeta tafrani na kuzua mgogoro mkubwa....sasa Fanyeni hili
ReplyDelete1. Kwakuwa tarehe ya mwisho kuchukua fomu as kugombea Uongozi katika uchaguzi uliotishwa ni tarehe 13. Mmoja wa wanachama aende kumchukulia form Manji.
2. Kamati ya Utendaji ya Yanga ifanye juu chini ikutane na Kamati ya TFF ya uchaguzi ndani ya masaa 48 ili kutoa mwongozo kwamba nafasi zinazotakiwa kugombea ni hizo zote isipokuwa ya Mwenyekiti kwani ameandika barua kuwa anarejea.
cha msingi uchaguzi ufanyike kwa mujibu wa katiba kwa kuwa Kipindi/ukomo wa miaka 4 umepita !
ReplyDelete