Mkali wa pasi za mwisho kwa sasa Ligi Kuu Tanzania Bara,
Ibrahim Ajibu amekataa mabao yake aliyofunga Ligi Kuu na kumwachia kocha Mkuu wa Yanga, Mwinyi Zahera mabao pamoja na pasi zake.
Ajibu amefanikiwa kufunga mabao 5 kwenye Ligi Kuu pamoja na kutengeneza pasi za mwisho 13 zilizozaa mabao huku akitumia zaidi mguu wa kulia kufuga na kutoa pasi za mwisho.
Ajibu amesema kuwa mafanikio yake yanabebwa na maelekezo ya kocha pamoja na ushirikiano uliopo ndani ya kikosi cha Yanga ambacho kwa sasa kinaongoza ligi kikiwa na pointi 47.
"Maelekezo ambayo napewa na kocha ndiyo yanayosaidia kuweza kupata matokeo, tunatambua kwamba kila mechi kwetu ni muhimu kupata matokeo na tunapambana mpaka kupata matokeo.
"Nazingatia sana mazoezi kwani huwezi kuwa bora kama haufanyi mazoezi, natumia muda mwingi kufanya mazoezi kwa ajili ya kujiandaa na michezo yetu inayofuata, mashabiki watupe sapoti," alisema Ajibu.
Yanga wamecheza michezo 17 na kufanikiwa kushinda michezo 15 na sare 2 ni vinara kwenye msimamo wakiwaacha Simba kwa jumla ya pointi 17 wakiwa wamecheza michezo 13.
0 COMMENTS:
Post a Comment