Simba itakuwa inashuka dimbani kukipiga na mashetani hao ukiwa ni mchezo wa marudiano baada ya ule wa awamu ya kwanza kumalizika kwa kufungwa mabao 2-1 ugenini.
Kuelekea mechi na Nkana, Simba leo itakuwa na kibarua cha ligi kucheza na KMC kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Kipute cha leo na KMC kimefanya Mbelgiji Aussems kubadili aina ya wachezaji ambao atawatumia ili kuwapa nafasi wale nyota Jumapili dhidi ya Nkana.
Imeelezwa kuwa Mbelgiji atawatumia wachezaji wengi zaidi ambao hawachezi katika kikosi cha kwanza kwa hofu ya kutoumia kabla hawajakutana na miamba hiyo ya Zambia.
Ni yaleyale sportspesa ya mwaka jana walipotumiwa wachezaji wa akiba na kuyaona matokei
ReplyDeleteMbona hawakutajwa hao wataoshiriki?
ReplyDeleteAmewataja wapi kanjanja?
ReplyDeleteAnazingua! Lakini pia, tatizo la Kocha wetu ni kutokuwa na mfumo mbadala wa uchezaji, hivyo hata akiwabadilisha wachezaji kama ni lengo Nkana wasiwasome wachezaji watakaokutana nao, bado tatizo litabaki kwenye mfumo wa uchezaji, hawezi kubadilisha uchezaji, hivyo, Nkana wataisoma Simba kwa aina ya mfumo tu. Mbinu ni zile zile tu. Hata angeazima wachezaji wa Kagera sugar na kuwakochi kwa siku moja, bado angewafundisha mbinu na mfumo ule ule tu atakaoutumia kwa Nkana. Hivyo, kwa upande wangu mimi naona hii mechi ya KMC itabidi TFF wajifunze kupitia matokeo baada ya mechi na NKANA.
ReplyDeleteHapo kuna kitu kitatokea kama c kupoteza mechi na KMC basi itakuwa na Nkana kumbuka KMC haina pressure kama Simba.
ReplyDeleteMwandishi kanjanja sana,pu.....mbavu,WAP hao wachezaji,nimewavumilia sana,Leo ndio mwisho kutumia blog yenu,nilidhan mmejirekibisha,wehu kabis nyinyi
ReplyDelete