YANGA YAPOKEA MAMILIONI YA FEDHA ARUSHA
Baada ya kutua salama jijini Arusha jana, wadau na wanachama wa klabu ya Yanga wameamua kuwekeza nguvu zao kwa kuichangia timu kiasi cha shilingi za kitanzania, milioni 8.
Wanachama na wadau hao wenye mapenzi ya dhati na Yanga, wametoa kiasi hicho cha pesa kwa ajili ya kuipa hamasa na kuisaidia baadhi ya gharama za kutumia kwa kipindi cha siku tatu ambazo itakuwa mkoani humo.
Yanga imewasili Arusha kwa ajili ya mechi na African Lyon itakayopigwa kwenye Uwanja wa Sheikh Amri Abeid majira ya saa 10 kamili jioni siku ya Alhamis.
Mashabiki hao wamejitoa kuisaidia Yanga kulingana na wakati mgumu inaopitia hivi sasa baada ya kuyumba kiuchumi tangu kuondoka kwa aliyekuwa Mwenyekiti wake, Yusuf Manji.
0 COMMENTS:
Post a Comment