December 19, 2018


Hii inaweza kuwa pengo. Unaambiwa kiungo fundi na anayekuja kwa kasi ndani ya kikosi cha Yanga, Feisal Salum ataukosa mchezo wa kesho dhidi ya African Lyon jijini Arusha.

Yanga itashuka dimbani Sheikh Amri Abeid ikiwa mgeni wa Lyon kuendeleza harakati za kuusaka ubingwa wa ligi ambao ilipokwa na Simba msimu uliopita.

Salum maarufu kama Toto atakosekana kutokana na kuwa na idadi ya kadi tatu za njano ambazo zitamfanya asubiri mpaka mchezo mwingine ujao wa ligi.

Kukosekana kwa Toto kunafanya idadi ya wachezaji tegemo Yanga kuwa nje ukiachana na Andrew Vincent, Rafael Daud ambao ni majeruhi pia Papy Tshishimbi ambaye amesafiri kuelelekea kwao baada ya kufiwa na mkwe wake.

Mabingwa hao wa kihistoria hapa Tanzania kwenye ligi watakuwa wanasaka alama zingine tatu bila nyota wake wakiwa kileleni mwa msimamo wa ligi na alama 44.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic