December 4, 2018

Kocha Mkuu wa Simba, Patrick Aussems amesema anawatambua vizuri wapinzani wake Mbabane Swallows ambao atacheza nao leo hivyo hesabu yake kubwa ni kuweza kupata ushindi wa mapema.

Simba watacheza leo na Mbabane katika mchezo wa marudiano wa Ligi ya Mabingwa Afrika baada ya ule wa kwanza uliochezwa uwanja wa Taifa kuweza kuibuka na ushindi wa mabao 4-1.

"Tunajua kwamba tupo ugenini na haiwezi kuwa mechi rahisi kwetu kwa kuwa wapinzani wetu wanataka kuonyesha kuwa wapo nyumbani ambapo ni muhimu kuibuka na ushindi kwa upande wao, kikubwa kwetu ni kupata ushindi wa mapema ili kuwachanganya wapinzani," alisema.

Simba watavaana na Mbabane katika uwanja wa Mavuso Sports Center, Manzini nchini Eswatini.

1 COMMENTS:

  1. Ushindi ni furaha kwa wanasimba wrote na wapenda mpira mzuri

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic