December 1, 2018


Mlinda  mlango wa timu ya Azam FC iliyo chini ya kocha mkuu Hans Pluijm, Metacha Boniphace amejiunga na timu ya Mbao FC kwa mkopo na kufikisha idadi ya wachezaji watano kutolewa na klabu ya Matajiri Tanzania.


Mwenyekiti wa Mbao FC, Solly Njash amesema kuwa wamejipanga kuimarisha kikosi chao ili kuweza kuleta ushindani ndani ya ligi.

"Tumemrejesha Boniphace katika kikosi chetu katika mashindano ambayo tutashiriki ikiwa ni pamoja na SportPesaCup, mashabiki waendelee kutupa sapoti," alisema.


Mratibu wa Azam FC, Philip Alando alisema kuwa wamefanya hivyo kuwapa nafasi wachezaji wao ili kuendelea kukuza vipaji vyao.


Wachezaji wengine ambao waltolewa kwa mkopo ni pamoja na Ditram Nchimbi ambaye yupo Mwadui FC, Wazir Junior Bisahara United, Abdul Haji yupo Mbao na Mbaraka Yusuf Namungo ya daraja la kwanza.





0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic