December 1, 2018

Kikosi cha Mtibwa Sugar kinatarajiwa kuifuata kibabe kesho Northern Dynamo ya Shelisheli kikiwa na wachezaji 18 kwa ajili ya mchezo wa marudiano uliopangwa kufanyika jumanne ijayo.

Mtibwa inakumbukumbu ya kushinda mchezo wao wa nyumbani kwa mabao 4-0 ukiwa ni mchezo wa kwanza wa Kombe la Shirikisho Afrika, wanatakiwa kutoruhusu kufungwa ili waweze kupenya kwenye hatua ya awali.


Ofisa habari wa Mtibwa Sugar, Thobias Kifaru amesema kuwa taratibu za usafiri zimekamilika ambapo wachezaji 18 na viongozi saba wanatarajiwa kuondoka kwa ndege itakayopitia Dubai kisha Shelisheli kwenye mechi hiyo.


"Timu inaondoka nchini kesho, tunapitia Dubai kisha tunaenda Shelisheli ambapo tutafika Desemba 3, siku inayofuata tutacheza mechi baada ya hapo timu itabaki hadi siku inayofuata na tutarejea Desemba 6, mwaka huu," alisema.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic