December 28, 2018


Imeripotiwa kuwa kiungo mpya wa Yanga aliyesajiliwa kutoka Mtibwa Sugar, Mohammed Issa 'Banka, ameanza mazoezi binafsi huko visiwani Zanzibar.

Banka ameanza mazoezi hayo baada ya kupewa ruhusa maalum walau kujiweka fiti kulinda kiwango chake.

Mchezaji huyo alifungiwa kifungo cha miezi 14 ambapo kitamalizika Februari 8 mwaka ujao kutokana na kubainika kutumia dawa ambazo haziruhusiwi michezoni.

Banka ambaye ni mchezaji wa kikosi cha timu ya taifa ya Zanzibar atafanya mazoezi binafsi mpaka pale kifungo chake kitakapomalizika.

Kiungo huyo ataendelea na mazoezi hayo bila ya kucheza mchezo wowote wa soka kwa mujibu wa kifungo alichopewa baada ya kufungiwa.



0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic