December 28, 2018


Wakala wa mchezaji Mtanzania Mbwana Samaata anayekipiga katika timu ya KRC Genk huko Ubelgiji, Jamali Kisongo, amewataka watanzania kuwa na subira juu ya hatma ya mchezaji wake kama atasajiliwa na timu zingine za ulaya.

Kisongo amesema watu wanapaswa kuwa na subira kutokana na tetesi mbalimbali zinazoendelea kutolewa mitandaoni kuwa Samatta anatakiwa na timu mbalimbali huko ulaya.

Kauli ya Kisongo imekuja mara baada ya klabu ya Middlesbrough inayoshiriki Championship nchini England kuanza kumhusisha Samatta ikitaja kumsajili, lakini Kisongo hajataka kuliweka suala hilo wazi kwa kina.

Hata hivyo, Wakala huyo ameeleza suala la Samatta kuongeza mkataba na Genk halina maana kuwa ataendelea kusalia hapo milele.

Kisongo ameeleza inategemeana na mkataba wenyewe unasema nini hivyo uwezekano wa kuvunjwa na kumfanya akaelekea sehemu nyingine inawezekana.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic