December 7, 2018






Kocha Mkuu wa Yanga, Mwinyi Zahera amesema anatambua ugumu wa kucheza na timu ambayo ipo kwenye nafasi ya chini hasa ligi kuu kutokana na namna zinavyopambana kusaka matokeo zikiwa uwanjani.

Zahera ana kumbukumbu ya kukutana na ugumu wa kupindua matokeo kibabe katika mchezo wake dhidi ya Tanzania Prisons ambao alifanikiwa kushinda kwa mabao 3-1 kwa kuwa Prisons ni miongoni mwa timu iliyo nafasi za chini.

"Kuna ugumu kucheza na timu zilizo chini kwenye msimamo hivyo kazi kubwa ambayo wachezaji wanayo ni kuona wanapata matokeo na kuiheshimu timu ya Biashara United tutakayocheza nayo Jumapili," alisema.

Biashara United wanashika nafasi ya 20 kwenye ligi kuu wakiwa wameshinda mchezo mmoja sawa na Tanzania Prisons ambao wapo nafasi ya 19 wakiwa na pointi 10.

2 COMMENTS:

  1. Biashara haina ugumu wowote mbele ya Yanga tena Daresalam. Ni kibonde tu na atachezea zaidi ya goli nne saaafi.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic