December 7, 2018



Mabingwa watetezi wa Ligi Kuu Tanzania Bara na wawakilishi katika michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika Simba, wameanza kujiandaa kwa ajili ya kuwavaa Nkana FC katika mchezo wa hatua ya kwanza utakaopigwa Desemba 14 Zambia.

Simba wameanza mazoezi leo katika uwanja wa Boko wakiwa chini ya kocha mkuu raia wa Ubelgij Patrick Aussems ambaye hesabu zake kubwa ni kupata ushindi wa mapema.

Aussems amesema kuna kazi kubwa kupata ushindi ila inawezekana kwani hicho ni kipambele namba moja kwa wachezaji wake na timu kiujumla.

"Tunatambua tuna kazi ngumu ya kufanya ili kupata matokeo hilo lipo wazi ila imani yetu tutafanikiwa kushinda ili kusonga mbele, mbinu mpya na kujiamini kwa wachezaji wangu kunanipa furaha," alisema.

Simba walifanikiwa kutinga hatua hiyo baada ya kuifunga mabao 8-1 Mbabane Swallows ambapo mchezo wa nyumbani walishinda mabao 4-1 na marudiano nchini Eswatini walishinda mabao 4-0 huku Nkana FC ya Hassan Kessy wana jumla ya mabao 3-1 walicheza dhidi ya UD Songo.

4 COMMENTS:

  1. Sisi Watanzania tunataka nini?
    Kuna watu sasa au waandishi au vyombo vya habari wanasema chama hastahili kucheza ligi yetu anapoteza muda wake. Angepaswa kuwepo Africa kusini au kwengineko lakini si Tanzania nadhani hata watu wangepata nafasi kuzungumza nae wangemuambia ni mjinga kaja kufanya nini hapa. Kweli sisi watanzania hatustahili vizuri? Kwanini sisi watanzania tunakosa kujiamini kiasi hicho? Vipi Mwinyi Zahera wa Yanga anastahili kupoteza muda wake pale Yanga? Ninachokiamini mimi chama anastahili kabisa kucheza ligi yetu na yupo mahala salama pale Simba kama riziki ipo basi Chama atasonga mbele zaidi. Wazambia wanajulikana kwa ubora wao kwenye soka ila watanzania sisi ni wanafiki sana kiasi cha kutia kichefuchefu. Hao wanaoponda Chama kuja kucheza ligi yetu ndio waliokuwa wakipiga kelele za dharau kuwa wachezji wengi wa kigeni wanaokuja kucheza ligi yetu hawastahili kucheza kwakuwa hawana viwango. Labda chama angekuwa anachezea Yanga angestahili kuchezea ligi yetu licha uwezo wa Yanga wa kumtunza mchezaji kama Chama kwa sasa ni kujitafutia mateso yasio ya lazima. Ninachokiamini mimi Tanzania Azam na Simba zinaonesha njia kuwa Tanzania tunaweza kupiga hatua tukiamua kama ilivyo upigwaji hatua mzuri wa maendeleo katika taasisi nyengine za umma hapa nchini hivi sasa. Tatizo la mpira wetu bado hatujawa na taasisi imara inayosimamia mpira nchini lakini kuna watu wanapambana kuuwinua mpira wetu na wanapaswa kutiwa moyo na kuungwa mkono na kupongezwa.

    ReplyDelete
  2. Mkubwa umenena, huwa hatuthamini mafanikio ya wenzetu, kila kukicha ni kuponda tuuuuu.

    Protas-Iringa

    ReplyDelete
  3. Ni kweli kabisa, watu wanapenda kusikia au kuona tunashindwa, lakini tena tukishindwa sisi wenyewe ndo wa kwanza kuusema uongozi uliohusika kusajili, uongozi uliopanga kikosi, na mengine mengi. Na pia kwa vie leo mazuri yapo Simba maneno ya kejeli yamekuwa meeeeeengiiiiii. Mara hao mliowafunga 8 ni vibonde, hv kweli mtu ambaye anaujua mpira wa Afrika kwa miaka hii anaweza kutamka utumbo kama huo! huu ni wendawazimu uliokithiri!. Mbambane Swallows ni timu kubwa yenye jina na yenye uwezo mkubwa kimpira na inacheza mpira wa kisasa kabisa sio kama hawa wapinzani wanavyosema. Siku zote usidharau kufeli kwa mtu ukasema hana uwezo, ni lazima umsifie kwanza yule aliyefaulu, maana ndo aliyesababisha umuone huyu kafeli, na pia unapomsifu mkimbiaji namba 1, usisahau kumsifu anayemfukuzia pia, maana uwezo wake ndo unamfanya huyu aliyeshinda aonekane kashinda. Tuache dharau jamani, na wala msitake kuwakatisha tamaa wachezaji wetu wa simba. Na hao NKANA tukiwachapa sijui mtasemaje!

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic