Kikosi cha Mbao FC, leo kitakuwa kazini kipambana na Dar City katika mchezo wa kombe la Shirikisho wakiwa na kocha mpya Ally Bushiri ambaye ni kocha Msaidizi aliyeajiliwa akitokea timu ya Njombe Mji ambayo ilishuka daraja na kwa sasa inashiriki Ligi Daraja la Kwanza.
Mshambuliaji wa Mbao Evagirtius Mujahukwi ambaye kwenye Ligi Kuu ana mabao 3 na yote aliyafunga akitokea benchi amesema wamejipanga kufanya kazi kubwa leo mbele ya kocha wao mpya.
"Kazi kubwa kwetu ni kutafuta matokeo tunajua kwamba moira ni dakika 90 hivyo tutapambana kufa na kupona ili kusonga mbele kwenye mashindano haya.
"Mbinu mpya ambazo kocha wetu ametupa zitasaidia kuweza kuibuka kidedea leo hatuna mashaka katika hilo na wapinzani wetu tunawaheshimu kikubwa ni kufuata maelekzo na akili ya mpira," alisema.








0 COMMENTS:
Post a Comment