Baada ya Mtibwa Sugar kupoteza mchezo wao wa hatua ya kwanza dhidi ya KCCA ya Uganda kwenye mashindano ya Kombe la Shirikisho uliochezwa nchini Uganda, Mtibwa Sugar wamepania kupindua meza kibabe kwa kupata ushindi leo.
Mtibwa Sugar walikubali kufungwa mabao 3-0 hivyo ili waweze kupenya kwenye hatua ya pili wanatakiwa washinde mabao 4-0 katika uwanja wa nyumbani ambapo watatumia uwanja wa Chamazi.
Kocha Mkuu wa Mtibwa, Zuber Katwila amesema anatambua kazi kubwa ambayo wanayo hasa baada ya kufungwa mabao 3 ila wana uhakika wa kupindua matokeo baada ya kujifunza kupitia makosa.
"Mpira ni mchezo wa makosa na unabebwa na mbinu ambazo zinasaidia kupata matokeo, wao waliweza kutushinda kwenye mchezo wao wa nyumbani basi nasi tunaweza kushinda katika mchezo wetu tutakaocheza nyumbani.
"Ushindani ni mkubwa nasi tupo tayari kupata matokeo, tunahitaji bao 4-0 ili tuweze kupenya imani yetu tunaweza kwa kuwa morali kwa wachezaji ni kubwa na makosa tumeyafanyia kazi, mashabiki watupe sapoti," alisema.







0 COMMENTS:
Post a Comment