December 7, 2018


Bao la Jacob Masawe dakika ya 38 wa Stand United limewalaza Singida United leo katika uwanja wao wa nyumbani wa Namfua uliopo Singida walipowakaribisha 'Chama la wana' kutoka Shinyanga.

Singida United wanapoteza mchezo wao wa 7 kati ya 15 waliyocheza mpaka sasa wakiwa na pointi 18 baada ya kushinda michezo 5 na kutoa sare michezo mitatu.


Kwa mujibu wa Mkurugenzi wa Singida United, Festo Sanga amesema kuwa mapito haya ni kwa muda tu kwa kuwa sasa wapo kwenye mikakati ya kuboresha kikosi chao ambacho kinakosa washambuliaji makini.


"Tunapita katika wakati mgumu ambao ni wa muda tu imani yetu tutafanya vizuri mara baada ya kusajili wachezaji wazuri watakaoongeza nguvu katika timu yetu," alisema.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic