December 7, 2018



Kocha Mkuu wa Yanga, Mwinyi Zahera amesema kuwa mchezaji wake Kelvin Yondani, ambaye hakuwa na timu kwenye michezo waliyocheza kanda ya Ziwa pamoja na Mbeya kutokana na kile alichoeleza kusumbuliwa na majeruhi ya enka.
 
Yondani ni nahodha wa Yanga alikosa mechi tatu ambazo Yanga walicheza na walifanikiwa kuchukua pointi 9 katika mechi hizo ambazo ni dhidi ya Mwadui FC, Kagera Sugar na Tanzania Prisons.

Zahera amesema kuwa tayari amempokea Yondani na ameanza mazoezi na wachezaji wenzake kuelekea katika mchezo wao dhidi ya Biashara United utakaochezwa jumapili kwenye uwanja wa Taifa.

"Yondani ni miongoni mwa wachezaji ambaye nitamtumia katika mchezo wetu dhidi ya Biashara United, najua watakamia kucheza nasi hasa kutokana na nafasi yao ambayo wapo hivyo nimewaambia wachezaji wawe makini kutafuta matokeo," alisema Zahera.

Yanga imecheza michezo 14 mpaka sasa bila kupoteza hata mchezo mmoja watakutana na Biashara united ambao wameshinda mchezo mmoja tu kati ya 14 waliyocheza mpaka sasa.

1 COMMENTS:

  1. hivi Yanga hawana daktari wa timu hadi mchezaji ajitibie mwenyewe bila viongozi na makocha kujua

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic