DIMPOZ ATOLEWA HOSPITALI NCHINI UJERUMANI
MUNGU mkubwa! Ndivyo unavyoweza kusema baada ya staa wa Bongo Fleva, Omary Nyembo kutolewa katika hospitali ya University Hospital of Dusseldorf ya nchini Ujerumani alikokuwa amelazwa baada ya kupata nafuu na kupelekwa Mombasa nchini Kenya.
Baba mzazi wa staa huyo, Faraji Nyembo alisema anamshukuru Mungu na Watanzania kwa maombi yao kwani mwanaye huyo kwa sasa ana nafuu na amepelekwa Kenya kwa ajili ya kuhudhuria kliniki.
Aliendelea kueleza kuwa kwa sasa afya ya Dimpoz imeendelea kuimarika ambapo amefanikiwa kuruhusiwa kutoka hospitali ikiwa ni baada ya kufanyiwa oparesheni kubwa ya koo na sasa yupo nchini Kenya anakofanya kliniki pamoja na kupumzika pia.
“Mwanangu sasa anaendelea vizuri kwani upasuaji aliofanyiwa umempa nafuu na hivi ninavyoongea na wewe ameruhusiwa kutoka hospitali nchini Ujerumani na yupo Kenya anakofanyia kliniki yake akisimamiwa na meya wa Mombasa ambaye ndiye anayempatia msaada wa matibabu,”
“Watanzania waendelee kumuombea Dimpoz ili arudi kama zamani kwani anavyoendelea kwa sasa ni matumani yangu atapona haraka na kurudi kwenye hali yake ya kawaida,” alisema Baba Dimpoz.
TUJIKUMBUSHE
Dimpoz alianza kuugua mapema mwaka huu ambapo kwa mujibu wa taarifa za madaktari wa Afrika Kusini alipokwenda kufanyiwa upasuaji wa kwanza, msanii huyo alikunywa sumu iliyowekwa kwenye kinywaji na kumsababishia koo kuziba.
Kabla ya kwenda Afrika Kusini alianza kupatiwa matibabu hapa nchini baadaye Kenya ambako madaktari walishauri upasuaji huo wa kwanza ufanyike huko Afrika Kusini kutokana na uzito wa tatizo lake, upasuaji wa awali ulifanyika vizuri akapata nafuu na kurudi nchini lakini hali ilibadilika tena hivi karibuni na kupelekwa nchini Ujerumani na kufanyiwa upasuaji wa pili.
Mungu ampiganie
ReplyDelete