December 22, 2018


Mpira umemalizika katika Uwanja wa Chamanzi jiji Dar es Salaam kwa Mtibwa Sugar kupokea kipigo cha mabao 2-1 kutoka kwa KCCA ya Uganda. 

Mechi hiyo ya Kombe la Shirikisho Afrika inawaaga rasmi Mtibwa kwa kipigo cha jumla ya mabao 5-1.

Ikumbukwe Mtibwa ilifungwa mabao 3-0 katika mchezo wa kwanza uliopigwa nchini Uganda wiki iliyopita.

Kesho kutakuwa na mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika ambapo Simba SC watakuwa wanawakaribisha Nkana Red Devils ya Zambia kwenye Uwanja wa Taifa Dar es Salaam.

2 COMMENTS:

  1. Mtibwa Yanga? Inaonekana muandishi bila ya kuitaja Yanga inakuwa tabu. Ukija kwa upande wa Mtibwa kutolewa kwenye mashindano ni dhahiri Mtibwa wamevuna kile ambacho walikipanda hasa kuhusiana na suala la usajili. Na kama kweli Watanzania tulikuwa tunataka kujipima uwezo wa wachezaji wa ndani basi Mtibwa ilikuwa ni kipimo tosha.Mtibwa ni asilimia mia moja 100% wazawa kuanzia wachezaji mpaka benchi la ufundi hivyo nnaimani watanzania tutakuwa tumejifunza kitu hapo. La kushangaza kesho yake hao makocha wa Mtibwa wamekabidhiwa timu ya Taifa? Watanzania tuwache utani kwenye kazi za watu.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Ww Acha Kumlaum "Mwandishi Wa Habari" Yanga Inatoka Wapi Hapa Au Haujasoma Vizuri Mbona Hapa Kaizungumzia Mtibwa Tu Na Simba Kesho Au Labda Umejisahau Ukajua Anazungumuzia Ligi Kuu Ambayo Ninyi Yanga Mnashiriki Mzee Baba Ni Ligi Ya Mabingwa Africa Na Shirikisho Sasa Kesho Kama Huwezi Kufika Taifa Azam Sport 2 Mbashara Kama Kawa Saa Kumi Jion

      Delete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic