EXCLUSIVE: BOBAN SASA NI WA KIJANI NA NJANO
Aliyewahi kuwa mchezaji wa Simba SCm Haruna Moshi 'Boban' amejiunga rasmi na Yanga kwa kusaini mkataba.
Boban amemwaga wino rasmi baada ya kuwepo kwa taarifa zilizoshika kasi kwa takribani miezi kadhaa kuwa Yanga ilikuwa mwenye mazungumzo naye.
Mchezaji huyo amejiunga na Yanga akiwa anatokea African Lyon ya Dar es Salaam.








Mmechemka mtaleta mgogoro mkubwa sana....tafadhali rekebisheni hili....huyu mchezaji hana kitu....Kocha Zahera utaanza kulaumiwa kwa udhaifu wa viongozi...numbs litakuangukia kwani wakina Nyika wanasema ni ushauri wa Kocha....Takukuru iingilieni hili na kuchunguza kwanini wanaleta wachezaji kutoka nje lakini hawasajiliwi? GHARAMA za Hoteli, visa na kuishi hizi nani anazilipa na hawa wageni wanakuja na kuondoka kiholela...
ReplyDeletewakati anasajiliwa ngasa mliongea upumbafu kama huo lakini leo hii ngasa ni msaada kwa yanga.......pambaneni na hali zenu ya yanga waachieni yanga wenyewe.
DeleteNa kwa ngasa mliongea hivyo hivyo sasa kaen kwa kutulia
DeleteNa kwa ngasa mliongea hivyo hivyo sasa kaen kwa kutulia
DeleteNadhani Yanga wanaanza kuonesha ni jinsi gani hawajiemdeshi kisayansi upuuzi gani kusajili huyu Mzee alijichokea
ReplyDeletekama boban unamuona mzee mbona kuna wachezaji wamemzidi umri wapo simba na yanga(yondani,kagere,wawa)hamjawaona wazee.....acha ushabiki wako maandazi....ongea fact.
DeleteIngekuwa timu nyingine imemsajili....ungesikia ohh wamesajiliwa wazee...eti wahenga!
ReplyDeleteKagere jr
Deletewahenga ndio......kwani kagere na wawa si wamemzidi umri boban.....au hujui!!!!!??
DeleteBoban sio mzee ana umri kama kina Kagere
ReplyDeletekagere mkubwa.....kamzidi boban mwaka mmoja.....boban 1987 kagere 1986
DeleteThis comment has been removed by the author.
ReplyDeleteUshenzi kabisa huu but anyway mbuzi anakula kutokana na urefu Wa kwamba yake
ReplyDeletepambaneni na hali zenu......ya yanga hayawahusu....waachieni wenyewe......mlisema timu mbovu na haina hela lakini leo tunawaongoza wenye timu bora na wenye hela
DeleteHaaaah
ReplyDeleteMchezaji bado mzuri ila sasa mjue, pesa ya mshahara au ya usajili ya Boban hailali nje. Atasumbua huyu na hatishwi na Kocha anapodai chake bora Kakolanya ana nafuu
ReplyDeleteheeeeh heeeeh heeeh
Deleteila akishindwa kuwika kwenye mechi ya simba na yanga msianzekumsema kuwa ni kirusi cha simba
ReplyDeleteMamluki wa Simba
ReplyDeleteKwako Kocha Mwinyi Zahera...kuna upungufu wa makipa ..beno kagoma na ameandika barua ya kuvunja mkataba na kwahiyo unatakiwa ushauri asajiliwe kipa mwingine....USIJE UKAWADHARAU WANA YANGA UKASEMA WAWILI WANATOSHA....SASA HIVI WANAKUSIFIA KESHO WATAKUVURUMISHIA MATUSI NA KUKUCHAPA BAKORA....UNAKATAA WACHEZAJI WAZURI NA KUISHIA KUSAJILI MAGARASA!
ReplyDeleteMsajili Faroukh shikalo kipa wa Harambee Stars....kabla ya Ijumaa!
Deletehayakuhusu......katoe ushauri kwa kocha wako wa simba
DeleteWanayanga tuukubali uamuzi wa kocha. Nani alijua kwa kikosi tulichonacho tungekuwa katika nafasi hii leo? Mpeni kocha nafasi yake kama kocha.
ReplyDeletendio manake.....yeye ndiye mwenye taaluma yake na ndiye anayepaswa kuchagua mchezaji anaeona anafaa kufanyanae kazi......nashangaaa wapumbavu wachache wao ndio wanajifanya wanajua kuliko kocha.
DeleteMimi namkubali bobani kiuchezaji , lakini kinidhamu atasumbua benchi la ufundi . na viongozi wajiandae kisaikolojia kwani hakopwi si fedha ys usajiri hata kukosa mshahara wa mwezi mmoja tu kwake anasepa na kuzua mgogoro .Acha tupambane na hali yetu
ReplyDeleteHaruna aliyepewa jina la utani Boban kutokana na kufananishwa kiuchezaji na kiungo wa zamani wa kimataifa wa Croatia na AC Milan, Zvonimir Boban ambaye kwa sasa ni Katibu Msaidizi wa Shirikisho la Soka la Kimataifa (FIFA), alizaliwa mwaka 1987 mjini Tabora, yaani anazidiwa na wote, Mnyarwanda Meddie Kagere na Muivory Coast, Serge Wawa Pascal wa Simba SC waliozaliwa mwaka 1986.
ReplyDeleteKisoka aliibukia Tabora kabla ya kujiunga na sekondari ya vipaji maalum vya wanamichezo, Makongo mjini Dar es Salaam mwaka 2001 na mwaka 2002 akasajiliwa kwa mara ya kwanza na klabu ya Ligi Kuu, Coastal Union ya Tanga akiwa ana umri wa miaka 15 tu.
Alidumu kwa msimu mmoja huko kabla ya kujiunga na Moro United mwaka 2003 alikocheza hadi 2004 alipohamia Simba SC ambako alicheza hadi mwaka 2010 alipouzwa Gefle IF ya Ligi Kuu ya Sweden.
Hata hivyo, katika mastaajabu ya wengi, pamoja na kukubalika Ulaya, Boban alirejea nyumbani Tanzania mwaka 2011 na kusiani tena Simba SC.
Baadaye alikwenda Oman kujiunga na Muscat Club kabka ya kurejea tena SImba SC ambako mwaka 2012 aliachwa kwa kile kilichoelezwa utovu wa nidhamu naye akaenda kujiunga na Coastal Union ya Tanga.
Alicheza Coastal Union kwa msimu mmoja kabla ya kuhamia Mbeya City ambako nako pia hakudumu akarejea Dar es Salaam kuchezea timu ya Daraja la Kwanza, Friends Rangers kabla ya msimu huu kujiunga na African Lyon aliyoichezea katika mzunguko wa kwanza wa Ligi Kuu hadi kumvutia kocha Mkongo wa Yanga, Mwinyi Zahera.
Boban amekuwa mchezaji wa timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars tangu mwaka 2004 ingawa kwa vipindi tofauti amekuwa akiachwa kwa sababu za utovu wa nidhamu na tangu mwaka 2009 baada ya Fainali za CHAN nchini Ivory Coast hakuwahi kuitwa tena Taifa Stars.
Ni kipenzi cha mashabiki wengi wa soka nchini akitukuzwa kama mmoja wa wachezaji wenye vipaji vya kipekee, ingawa wakati wote tuhuma za utovu wa nidhamu zimekuwa zikimuwekea mazingira magumu ya kikazi.