December 1, 2018


Baada ya kufikisha jumla ya mabao 7 mshambuliaji wa Yanga, Herieter Makambo amemshtua mfungaji namba moja kwenye Ligi Kuu Tanzania Bara, Eliud Ambokile.


Makambo amefikisha mabao 7 kwenye Ligi Kuu sawa na washambuliaji wawili wa Simba, Meddie Kagere na Emmanuel Okwi hali inayofanya kuwe na vita kubwa ya mfungaji bora msimu huu.


 Ambokile amesema kuwa anajifunza mambo mengi hasa kupitia washambuliaji hao hasa namna wanavyopambana uwanjani hivyo hana wasiwasi endapo watampita.

"Wanafanya kazi kubwa uwanjani hivyo wanapata kile ambacho wanastahili kupitia wao nami pia najifunza ili kuendelea kuwa bora siku zote.


"Sina hesabu za kuwa mfungaji bora ila kazi yangu kubwa ni kuweza kuisadia timu kuweza kupata matokeo, nitafunga kila ninapopata nafasi nina amini kila kitu kinawezekana," alisema.


 Ambokile anaitumikia timu ya Mbeya City amekuwa akihusishwa kujiunga na Yanga katika dirisha dogo baada ya kocha kuvutiwa na uwezo wake ili aongeze nguvu kwenye safu ya ushambuliaji wa Yanga.




BONYEZA HAPA ===> SALEH JEMBE SPORTS
👆👆👆👆👆👆👆👆👆👆👆👆👆👆👆👆👆👆👆👆👆👆👆👆👆👆
Kwa wasomaji wa Blog yetu pendwa ya michezo akikisha una nifollow INSTAGRAM kwa kubonyeza link iliyopo hapo Juu tutakudodoshea Upates zote za michezo kuanzia sasa.

Asante


BONYEZA HAPA ===> SALEH JEMBE SPORT

1 COMMENTS:

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic